Familia ya Obama yamshukuru Drake

0
900

Washington D.C

WIKI iliyopita rapa anayetamba na wimbo wake wa ‘Life Is Good’ Aubrey Graham maarufu kwa jina la Drake, ametumia ukurasa wake wa Instagram na kuianika barua aliyotumiwa na familia ya aliyekuwa rais wa Marekani, Barack Obama.

Familia hiyo iliamua kumtumia barua ya kumshukuru kwa kitendo chake cha kumtakia heri ya kuzaliwa mtoto wao Sasha, mwaka 2017 ambapo mrembo huyo alikuwa anasherehekea kutimia miaka 16 ya kuzaliwa kwake Juni 7.

Mbali na kupita miaka miwili, Obama na familia yake ikaamua kumtumia barua hiyo kumshukuru jambo ambalo Drake limemfurahisha msanii huyo.

“Tunatumia nafasi hii kukushukuru kwa kutumia muda wako na kumtumia ujumbe wa kumtakia kila la heri Sasha kutimiza miaka 16 ya kuzaliwa kwake hapo 2017, tunadhani unajua jinsi gani tulivyo na furaha baada ya kuona ujumbe wako, tunakushukuru sana,” iliandikwa barua hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here