27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 7, 2023

Contact us: [email protected]

FAMILIA 1,000 IGUNGA KUNUFAIKA UFUGAJI KUKU

Na ODACE RWIMO,

ZAIDI ya  familia 1,000 za wafugaji wa kuku wa kienyeji wilayani Igunga   zinatarajiwa kunufaika na mafunzo  ya teknolojia rahisi ya ufugaji wa kuku, imefahamika.

Mafunzo hayo yatawasaidia kupambana na majanga yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi.

 Meneja wa Mradi wa Shirika la Exponetial Pass on the Gift  (EPOG ), John Toto alikuwa akizungumza kwenye hafla  kujadili masuala ya jinsia na upimaji wa VVU katika uwanja wa Sokoine.

Alisema mradi huo unafadhiliwa na Shirika la Mitamba la Kimataifa (Heifer International Tanzania) kwa ushirikiano na Halmashauri ya Wilaya ya Igunga.

Ulianza kutekelezwa wilayani humo katikati ya mwaka 2016 na unatarajiwa kumalizika mwaka 2019, alisema.

 Alisema  familia au vikundi vitakavyonufaika na mradi huo hadi ifikapo 2019  vitatoka  katika vijiji 10.

Alivitaja vijiji hivyo kuwa ni  Mbutu, Bukama, Mwabakima, Mwang’halanga, Ibutamisuzi, Igunga, Mwanzugi, Isugilo, Mgongoro na Makomero.

Toto alisema   watu 10 walipelekwa Chuo cha Kilimo na Mifugo Tengeru mkoani Arusha  ambako walifundishwa   utaalamu wa mifugo na ufugaji bora wa kuku wa asili.

 “Katika mradi huu halmashauri ya wilaya itatoa wataalamu wa jamii na mifugo   kuendesha mafunzo kwa wanavikundi wote kwa wakulima na wafugaji na tayari vikundi 10 kutoka katika vijiji hivyo vimeundwa,” alisema.

 Mkuu wa Wilaya ya Igunga, John Mwaipopo, alipongeza jitihada nzuri zinazofanywa na shirika hilo.

Alisema hatua hiyo italeta mwamko chanya wa  maisha kwa  kushiriki katika masuala ya  jamii ikiwamo utunzaji mazingira na kupinga vitendo vya unyanyapaa.

 Ofisa Mawasiliano wa Heifer International Tanzania, Mercy Nyanda alisema mradi huo ni mkombozi kwa wananchi   wilayani humo.

Alisema mradi  utawanufaisha katika uchumi na kuwaepusha na maambukizi mapya ya VVU na vitendo vya unyanyapaa katika familia zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,885FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles