23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Falz, Peruzzi, Seyi Shay wapamba ‘Man on fire’ ya Idahams

Lagos, Nigeria

Msanii wa kizazi kipya anayefanya vizuri nchini Nigeria, Idahams amefanikiwa kuvuka kikwazo cha maradhi ya Covid 19 kwa kuachia albamu fupi (Extended Play- EP) iitwayo ‘Man On Fire’ yenye jumla ya nyimbo saba zilizobeba ujumbe wa kuwafariji na kuwapa moyo watu wote kwenye kipindi hiki cha janga hilo.

Nyimbo zilizomo ndani ya albamu hiyo ni mchanganyiko wa aina mbalimbali za muziki ikiwemo Afro Pop, Rap na aina nyinginezo huku miongoni mwa nyimbo ni Ada na Man on Fire alizoshirikiana na wanamuziki wengine Falz, Shima Peruzzi na Seyi Shay.

Katika albamu hiyo, Idahams anaendeleza moto aliouwasha mwaka 2020 kwa kutoa nyimbo kali zaidi ya zile zilizopo kwenye albamu iliyopita Belle, God When na No One Else alioutoa mwaka 2018 ambao ulisababisha asainiwe na lebo kubwa za Universal Music na Grafton Records.

Katika EP hiyo, Idahams ameendelea kuonesha uwezo mkubwa wa namna anavyoweza kutunga nyimbo zenye mashairi mazito na kupikwa na maprodyuza bora kwa kuzingatia asili yake ya Kusini mwa Nigeria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,244FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles