28 C
Dar es Salaam
Monday, January 24, 2022

FAKHI AMEGEUKA LULU SIMBA, YANGA

KUNA msemo unaosema ukinicheka shambani nitakucheka sokoni, ni msemo wa Kiswahili ambao una maana kubwa. 

 Mapema mwaka huu klabu ya Simba iliamua kumwachia mlinzi wake wa kati, Mohamed Fakhi kwenda Kagera Sugar kwa mkopo ambao ungemweka nyota huyo msimu mzima katika kikosi cha wakata miwa hao.

Simba walifanya hivyo ili kulinda kipaji cha nyota huyo kutokana na kushindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha kocha Joseph Omog raia wa Cameroon.

Halikuwa jambo baya kwa wakati huo kwa pande zote mbili mchezaji na klabu ni jambo la kawaida ulimwenguni kote kushuhudia mchezaji anatolewa kwa mkopo ili kurudi katika kiwango chake cha awali au kuongezeka mara dufu.

 Hivi sasa nyota huyo amegeuka kuwa lulu na kuiteka klabu yake ya zamani kutokana na uwezo aliouonyesha katika mchezo ule na kuwadhihirishia kuwa amerudi katika ubora wake.

Sakata la kadi tatu za njano linalomhusu nyota huyo limekuwa mjadala kila mahali kutokana na awali kutolewa maamuzi ya awali na Kamati ya saa 72, lakini siku chache baadaye Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ilianza kupitia pingamizi la timu ya Kagera Sugar kuhusu kupokwa pointi zao.

 Fakhi ambaye alikuwa katika kikosi kilichoibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya kikosi chake cha zamani Simba, sakata lake limeendelea kuwagawa wadau wa soka ambao wanahoji suala lililotolewa maamuzi kurudiwa.

Si vibaya kwa suala hili kurudiwa ikiwa kama Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi ya Wachezaji iligundua udhaifu katika maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya saa 72 ambayo iliona kuwa nyota huyo ana makosa.

Swali linaloumiza kichwa ni kama kweli wamekosea ina maana kuna matatizo katika Kamati za Shirikisho la Soka nchini (TFF), hili ni shauri moja limegeuka kizungumkuti, kuna haja ya kurudia na mengine ili kujiridhisha.

Ikiwa TFF wameshindwa kujiamini wenyewe na kujikosoa sisi ni nani hadi tuwaamini, kuna haja ya kuzipitia upya na hukumu zilizopita chini ya Kamati ya saa 72.

 Jambo hili limeibua hisia tofauti kwa klabu za Simba na Yanga ambapo vijana wa Msimbazi wamekosa imani na Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji jambo ambalo ni hatari kwa afya ya soka letu.

Wakati watani wao wa jadi wakiwa hawana imani na Kamati ya saa 72 kuwa imejaa wanazi na mashabiki wa Simba.

Huku mjumbe wa Kamati ya utendaji wa klabu hiyo, Salum Mkemi, akiahidi kuwabeba Kagera kwa kuhofia kuwa watani wao wamefanya mchezo usio wa kiungwana.

Ikiwa mambo haya yanafanyika kwa klabu kubwa vipi kuhusu klabu ndogo ambazo haziwezi kupaza sauti, zitaendelea kuugulia maumivu hadi lini.

Shirikisho linapaswa kuzitathmini kamati zake katika hili ili kuondoa utata ambao umekuwa ukijitokeza mara kwa mara.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
176,415FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles