28.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Fainali VILEVILE CUP kupigwa Julai 6

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Hatimaye mashindano ya VILEVILE CUP yanatarajia kufikia tamati Julai 6, mwaka huu wakati ya vitongoji vya Mtuzu na Makore wakapotoana jasho kwenye uwanja wa Mwenge kijijini Butiama mkoani Mara.

Mratibu wa mashindano hayo, Magembe Jackton amesema mchezo unatarajia kuanzia saa 10 jioni, huku mgeni akitarajia kuwa Mkuu wa wa Wilaya ya Butiama, Mosses Kaigere.

Amesema pia mchezo huo utahudhuriwa na Chifu wa Wazanaki, Japheth Wanzagi na mamia ya wakazi wa Kijiji hicho.

Amesema mashindano hayo yaliyoanza Juni 16, mwaka huu yalishikisha vitongoji vya Makore, Mtuzu, Butasya, Ikorokomio,Kitanga, Muhunda na Nyamagembe yamekuwa na mafanikio makubwa kwa kukutanisha vijana wengi wenye vipaji.

“Tunategemea fainali hii itakuwa nzuri, maana Kuna wachezaji wameonyesha uwezo mkubwa katika mashindano haya.

“Lengo letu ni kumuenzi Mzee Jackton Nyerere maarufu Vilevile maana alikuwa mkulima stadi na mtu wa watu, kupitia soka tunaamini tutaendelea kumbuka mzee wetu na kumuenzi hii,”amesema Jackton.

Amesema mzee Vilevile ambaye enzi za ujana wake alikuwa mtu wa michezo, amefanikiwa kuacha watoto na wajukuu wanaocheza soka kwa kiwango kikubwa.

Akitoa mfano amesema, wajukuu kama Magwari, Yusufu kibiriti, Erick Kulwa, Julius Magembe, Kiboko Manyerere ni tegemeo kwa taifa letu kwa siku zijazo.

Amesema katika mashindano ya mwaka huu, mshindi wa kwanza atajipatia zawadi ya kombe la kubwa na mpira, wakati mshindi wa pili ataondoka na mipira miwili, mchezaji Bora atapata medali na mshindi wa tatu atapata mpira mmoja.

Mzee Vilevile alifariki dunia February 19, 2017 na kuzikikwa nyumbani kijijini Butiama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles