30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 30, 2023

Contact us: [email protected]

Facts Production kuuza filamu zake nyumba kwa nyumba

NiliyemchaguaNA HERIETH FAUSTINE

KAMPUNI ya Facts Production inatarajia kuanza kusambaza filamu yake mpya ya ‘Niliyemchagua’ kwa mfumo wa nyumba kwa nyumba.

Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Mohammed Kazi ‘Mudy Kazi’ alisema ameamua kufanya hivyo ili kutoa nafasi ya wasiopata muda wa kwenda kununua CD za filamu hiyo katika maduka makubwa waweze kununua wakiwa nyumbani kwao.

“Lakini pia tumeona ni vizuri kwa kuwa itasaidia kuwatambulisha wasanii wetu chipukizi ambao wana uwezo mkubwa kuliko wasanii wenye majina makubwa, lakini pia tumeona ni vema kama kazi hizi zitasambazwa na sisi wenyewe ili tuondokane na wingi wa filamu zinazosubiri nafasi ya kusambazwa na wasambazaji wenye majina makubwa,’’ alisema Mudy Kazi.

Aliongeza kwamba uuzaji huo wa nyumba kwa nyumba utaanzia jiji la Dar es Salaam, kisha utaelekea mikoa ya karibu, ukiwemo Pwani, Morogoro na Tanga.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles