25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

EWURA yawaasa mafundi umeme kujisajili

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (EWURA) imetoa wito kwa mafundi umeme kujisajili na kupata leseni kwa ajili ya kufanya kazi ili kuepusha majanga mbalimbali yanayoweza kutokea ikiwemo shoti kusababisha hasara ya vitu mbalimbali .

Akizumgumza na Mtanzania Digital Julai 7, jijini Dar es Salaam katika maonyesho ya sabasaba, Afisa Uhusiano wa EWURA, Tobietha Makafu amesema hadi sasa mafundi wenye leseni za EWURA ni zaidi ya 5,000 nchi nzima ambapo kiwango hicho ni kidogo ukilinganisha na mafundi waliopo nchi.

“Napenda kutoa wito kwa mafundi kujisajili EWURA ili wapate leseni kwani fundi ukikamatwa unafanya kazi bila leseni utatozwa faini isiyozidi milioni moja au kifungo kisichopungua miaka 5 au vyote kwa pamoja,” amesema Makafu.

Amesema EWURA inafanya kazi kidigitali hata uombaji wa leseni hiyo unafanywa kidigitali ili kuhakikisha kila mtu anapata huduma hiyo kwa haraka na bila usumbufu.

Amesema kuwa uwepo wa Ewura kwenye maonyesho ya sabasaba ni kutoa elimu kuhusu shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo.

Amesema wanasaidia mafundi umeme walioshindwa kujisajili kwenye mfumo kwa sababu tofauti ili waweze kujisajili na kupata leseni zao kutokana na ngazi ya elimu, ujuzi na daraja la leseni.

“Nitoe wito kwa mafundi kuja hapa kwenye maonyesho ili wasaidiwe kujisajili hapa tupo na mtu wa IT atawasaidia kujisajili bila malipo yoyote,” ameongeza Makafu.

Aidha, amesema kujiunga na kujisajili unapaswa kuingia kwenye tovuti ya EWURA na utakutana na mfumo wa LOIS kidigital ambao unaweza kuwasiliasha hapo malalamiko mbalimbali yanayohusiana na huduma zinazodhibitiwa na mamlaka hiyo ikiwemo na ucheleweshaji wa huduma za umeme maji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles