31.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 3, 2024

Contact us: [email protected]

EWURA yatangaza bei mpya za mafuta

* Bei za rejareja za dizeli na petroli zimeongezeka kwa Sh 60 kwa lita

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Mamlakaya Udhibiti wa Huduma za Nishati  na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya za mafuta ya Petroli, Diseli na Mafuta ya taa kwa mwezi Machi 2022 ambapo bei za rejareja za dizeli na petroli zimeongezeka kwa Sh 60 kwa lita (sawa na asilimia 2.42) na Sh 65 kwa lita sawa na asilimia 2.77 mtawalia.

Imesema bei hizo zingeweza kuwa juu zaidi kama Serikali isingechukua hatua ya kuahirisha tozo ya Sh 100 kwa lita kwenye bidhaa za mafuta ya petrol, dizeli na mafuta ya taa.

Akitangaza bei hizo Machi Mosi, 2022 mbele ya Waandishi wa Habari, jijini Dodoma Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Titus Kaguo amesema bei za rejareja na jumla za mafuta hayo yaliyopokelewa kupitia bandari ya Dar es Salaam zimebadilika ikilinganishwa na toleo lilopita la Februari 2, mwaka huu.

Amesema hizo bei za rejareja za dizeli na petroli zimeongezeka kwa Sh 60 kwa lita (sawa na asilimia 2.42) na Sh 65 kwa lita sawa na asilimia 2.77 mtawalia.

Amesema bei ya rejareja ya mafuta ya taa imepungua kwa Sh 83 kwa lita sawa na asilimia 3.63.

“Vilevile ikilinganishwa na toleo la mwezi uliopita bei za jumla za petroli na dizeli zimeongezeka kwa Sh 59.65 kwa lita sawa na asilimia 2.54 na Sh 64.45 kwa lita sawa na asilimia 2.95 mtawalia.

Amesema bei ya mafuta ya taa imeshuka kwa Sh 82.67 kwa lita sawa na asilimia 3.82.

Amesema bei za mafuta hayo kwa Mikoa ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara) zimeongezeka ikilinganishwa na bei zilizotolewa Februari 2, mwaka huu.

Amesema kwa Machi, 2022 bei za rejareja petroli na diseli zimeongezeka kwa Sh 165 kwa lita sawa na asilimia 6.88 na Sh 207 kwa lita sawa na asilimia 9.09 mtawalia.

“Vilevile ikilinganishwa na toleo la mwezi uliopita bei za jumla na rejareja petroli na dezeli zimeongezeka kwa Sh 164.76 kwa lita sawa na asilimia 7.26 na Sh 206 kwa lita sawa na asilimia 9.62 mtawalia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles