31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

EWURA yajipanga kuimarisha nishati ya mafuta vijijini

Na Yohana Paul, Geita

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wamebainisha wameweka mazingira rafiki kuhakikisha huduma ya mafuta yanapatikana nchi nzima ili kuimarisha huduma ya usafiri kwa vyombo vya moto vijijini.

Meneja wa Ewura Kanda ya Ziwa, Mhandisi George Mhina amebainisha hayo wakati akizungumuza na waandishi wa habari katika viwanja vya Bombambili mjini Geita yanapofanyika Maonyesho ya Tano ya Teknolojia ya madini.

Mhandisi Mhina amesema “Sisi Ewura kwa sasa tunahimiza sana ujenzi wa vitruo vya mafuta vijijini, ili kuepuka wananchi kutumia mafuta kwenye vidumu, na tumetengeneza kanuni mahususi kwa hiyo tumerahisisha vigezo na mashariti.

“Ndio maana ukiona vituo vya mjini huku gharama yakekujenga inaweza kuwa Sh milioni 300 mpaka 500, sasa kwa mtanzania wa kawaida kule kijijini ambako kuna bodaboda na shughuli zingine vigezo tumevirahisisha zaidi.

“Mtu akiwa na Sh milioni 40 mpaka 50, unaweza ukajenga kituo cha mafuta katika ngazi ya kijiji na wananchi wakapata mafuta bora na kwa gharama ambayo tunaipanga (bei elekezi).”

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Ally Gugu akizungumuza baada ya kukagua mabanda ya maonyesho hayo amesema Ewura ni miongoni mwa taasisi muhimu hivo waendelee kutekeleza wajibu wao.

“Wenzetu wa Ewura kazi yao kubwa ni kuhakikisha tunakuwa na nishati yenye viwango,ili tunapowavutia wawekezaji basi waweze kuja kuwekeza nchini na wapate huduma hizo zenye viwango ambazo wao wanazisimamia,” amesema Gugu.

Amesema Wizara inaunga mkono juhudi za Ewura kuhakikisha huduma ya mafuta inapatikana kila kona ya nchi hivo wameweka sera wezeshi kwa wawekezaji kujenga vituo vya mafuta vya chini, kati na vikubwa maeneo ya vijijini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles