30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Ewura yaitaka Tanesco kuondoa vikwazo kwa mafundi umeme

Na Derick Milton, Mwanza

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA) imelitaka Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kuondoa vikwazo kwa mafundi umeme ambao wamepewa vibali na Mamlaka hiyo kufunga mfumo wa umeme kwenye majumba ya watu.

Kauli hiyo imetolewa leo Februari Mosi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Mhandisi Godfrey Chibulunje wakati wa semina ya siku moja kwa Waandishi wa Habari Kanda ya ziwa kutoka Mikoa ya Simiyu, Mwanza, Mara pamoja na Geita.

Mhandisi Chibulunje amesema Shirika la Tanesco kwenye ofisi zake kila mkoa kumekuwa na utaratibu wa kuweka majina ya mafundi wanaowataka na kusema kuwa hao ndiyo mafundi ambao watahusika kutoa huduma katika eneo husika.

“Mfano ukienda Tanesco Mwanza au Simiyu utakuwa orodha ya mafundi na wanasema kuwa hawa ndiyo mafundi wanaotakiwa kufanya kazi katika mkoa huu, hii siyo sahihi hata kidogo, kumekuwepo na ukilitimba huu kwenye ofisi nyingi za mkoa na Wilaya.

“Hatua hii inakuwa kikwazo kikubwa kwa mafundi wengine wanaotoka nje ya mkoa husika, wanawawaweke vigingi ambavyo vinakiuka Sheria na taratibu, Ewura ikitoa leseni kwa fundi maana yake anatakiwa kufanya kazi sehemu yeyote ndani ya nchi na siyo mkoa fulani kuna mafundi hawa na mkoa mwingine wameweka wa kwao,” amsema Mhandisi Chibulunje.

Aidha, amesema kuwa ofisi yake inafanyia kazi changamoto hiyo, ambapo amelitaka Shirika hilo kuacha utaratibu huo na badala yake waache mafundi wafanye kazi sehemu yeyote ile ndani ya nchi kwani vibali walivyopewa vinawaruhusu kufanya hivyo.

Amesema kuwa Ewura imetoa vibali kwa mafundi zaidi ya 3000 ambao wanatosha kwa mahitaji ya nchi, ambapo ameitaka Tanesco kuwaacha wafanye kazi sehemu yeyote ya nchi na wasiwabagua au kuwa na mafundi wao wenyewe.

“Vibali vya hao mafundi vinatolewa na sisi kwa mujibu wa Sheria, lakini hili la Tanesco hatujui kwa nini wanalifanya na tutaguatilia kwani kufanya hivyo ni ukiukwaji wa Sheria, waondoe hivyo vikwazo, kila fundi aliyepewa kibali afanye kazi sehemu au mkoa, Wilaya yeyote,” ameongeza Mhandisi Chibulunje.

Amesema Mamlaka hiyo itafuatilia gharama za mafundi hao ambazo wamekuwa wakitoza wananchi wakati wa kuwafungia mfumo wa umeme kwenye nyumba zao kama siyo kubwa.

Pia amesema kuwa Ewura imefanikiwa kupunguza changamoto ya uchafuzi wa mafuta kutoka asilimia 80 mwama 2007 hadi kufikia asilimia 4 mwaka 2020.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles