EU yakubali kuongeza muda Brexit hadi Januari 31

0
484

LONDON, UINGEREZA

UMOJA wa Ulaya (EU) umekubali kuongeza muda wa Uingereza kujiondoa ndani ya umoja huo hadi Januari 31,2020.

Kwa mujibu wa andiko la tweeter lililotumwa na Rais wa Baraza la Ulaya, Donald Tusk umoja huo utaruhusu muda zaidi – maana yake ni kwamba Uingereza inaweza kujiondoa  kabla ya wakati iwapo tu mkataba utaidhinishwa na Bunge.

Hatua hiyo ya   EU imekuja wakati wabunge wa Uingereza wakijiandaa kupiga kura juu ya mapendekezo ya Waziri MKuu wa wa nchi hiyo, Boris Johnson kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mapema wa Desemba 12.

Vyama vya Scottish National  (SNP) na Liberal Democrat pia wamependekeza uchaguzi Desemba 9.

Andiko la muswada wa makubaliano la mabalozi 27 wa EU ambalo Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC linasema limeliona – pia linajumuisha  Mkataba wa Uingereza kuondoka EU kwamba hautaweza kujadiliwa tena katika siku zijazo.

Uingereza ilikuwa ilikuwa ijitoe EU keshokutwa, lakini Boris alitakiwa kuomba muda zaidi kutoka Umoja wa Ulaya baada ya Bunge kushindwa kuafiki mkataba wa Brexit.

Mara kadhaa Waziri Mkuu huyo wa Uingereza amekuwa akisema kuwa nchi yake itaondoka Oktoba 31 mwaka huu iwe au isiwe.

lakini kifungu cha sheria cha EU cha kujiondoa  kinayojulikana kama Benn – pia kinamhitaji akubali ‘ofa’.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here