23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

EU WASAIDIA MIRADI YA LISHE KANDA YA KATI

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula  Dunini (WFP), limepokea mchango wa Euro milioni 9.5 kutoka Umoja wa Ulaya (EU) kwa lengo la kuunga mkono mradi wenye thamani ya Euro milioni 24.5 (takribani Sh bilioni 50) kusaidia na kukuza usalama wa chakula na lishe katika mikoa ya kanda ya kati.

Mradi huo umeandaliwa ili kuimarisha usalama wa chakula na lishe kwa watu wapatao 40,000  na wakati huohuo ukichangia katika kupunguza utapiamlo katika wilaya zinazolengwa za Bahi na Chamwino mkoani Dodoma, Ikungi na Singida Vijijini katika Mkoa wa Singida.

Mchango wa EU ulitangazwa jana Dar es Salaam katika hafla ya kusaini makubaliano katika Jengo la Umoja jijini Dar es Salaam uliofanywa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya, Mwakilishi wa WFP Tanzania, Michael Dunford na Mkuu wa Ubalozi wa Umoja wa Ulaya nchini, Roeland Van De Geer.

“Licha ya kuimarika kwa viashiria vingi vya afya katika muongo uliopita, bado hakuna hatua kubwa katika kuimarisha hali ya lishe ya watoto na wanawake nchini Tanzania.  

 “Kuwapo viwango vya juu vya kudumaa, kukosa uzito wa kuridhisha na upungufu wa viinilishe nchini kunaashiria dharura ya kimyakimya. Utayari wa kisiasa katika safu ya viongozi wa juu katika kukabili lishe duni nchini Tanzania kwa mtazamo wa sekta nyingi kwa hakika ni mageuzi makubwa.

“Kupitia mradi huu, EU pamoja na WFP ziko katika nafasi nzuri ya kubaini na kuunga mkono uhusiano kati ya kilimo, afya, usalama wa chakula na lishe, ambao hapo kabla haukuwa umeelezwa kwa kina au kufuatiliwa kikamilifu,” alisema Van De Geer.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles