24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Ethiopia kuipiku Kenya kwa uchumi mkubwa

international_monetary_fund_logo-svg

NEW YORK, MAREKANI

UCHUMI wa Ethiopia unatarajia kuupiku wa Kenya baadaye mwaka huu, ikichangiwa na matumizi makubwa ya fedha katika ujenzi wa miundombinu.

Miundombinu hiyo mikubwa imelifanya taifa hilo la Pembe ya Afrika kuwa katika orodha ya mataifa yanayokuwa kwa kasi zaidi duniani kipindi cha miaka 10 iliyopita.

Takwimu mpya za Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) zinakadiria kuwa pato la ndani la Ethiopia (GDP) linatarajia kukua kutoka dola bilioni 61.62 mwaka 2015 hadi dola bilioni 69.21 mwaka huu, likilipiku lile la Kenya kwa tofauti ndogo.

Pato la ndani (GDP) la Kenya linatarajia kukua kutoka dola bilioni 63.39 hadi dola bilioni 69.17 kwa kipindi kama hicho.

“Ethiopia imeshuhudia ukuaji wa kiuchumi wa tarakimu mbili, ukiwa katika wastani wa asilimia 10.8 tangu 2005, kitu ambacho kimechochewa na maendeleo ya sekta ya umma,” inasema ripoti ya Benki ya Maendeleo Afrika.

GDP  la dola bilioni 14.1 mwaka 2000, lilikuwa kubwa kwa asilimia 71.6 dhidi ya lile la Ethiopia lililosimama kwa dola bilioni 8.23 mwaka huo. Hata hivyo, taifa hili la Pembe la Afrika limepunguza pengo kipindi cha miaka mitano iliyopita kutokana na ukuaji mzuri na wa kasi.

Kwa kuelekea kuipiku Kenya, Ethiopia itaimarisha nafasi yake kama eneo la kimbilio kwa wawekezaji.

Uwekezaji ulioisaidia Ethiopia kuwa taifa lenye nguvu kiuchumi ukanda huo, ni pamoja na miundombinu mikubwa ya umma kama ile ya China, ambayo imeliwezesha taifa hilo la Asia kuwa la pili kwa uchumi mkubwa  duniani kipindi cha miongo miwili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles