27.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 20, 2023

Contact us: [email protected]

ESSENCE OF WORSHIP kukiwasha Juni 16 Dar

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

Kundi la muziki wa Injili la ESSENCE OF WORSHIP limezindua Ibada ya uzinduzi wa Albamu ambayo wameipa jina la My Worship itakayofanyika Juni 16, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari kiongozi wa Essence of Worship, Gwamaka Mwakalinga amesema kuwa siku ya Ibada hiyo kutakuwa na waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili kutoka ndani na nje ya Tanzania.

“Mungu ametupa kibali cha kuandaa ibada maalumu ambayo tumeipa jina la my worship leo tunaitangaza rasmi kwani pia kwenye ibada hii kutakuwa na wasaniii mbalimbali kutoka ndani ya tanzania na nje tukae mkao wa kula chakula cha bwana,” amesema Mwakalinga.

Ameongeza kuwa ibada hiyo haitakuwa na kiingilio bali kutakuwa na utaratibu maalumu wa kushiriki ambapo watangaza katika mitandao yao ya kijamii na kuhusiana eneo watakalo fanyia ibada hivyo watatangaza hapo baadae.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles