27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 7, 2023

Contact us: [email protected]

ERDOGAN: KANSELA WA UJERUMANI ANATUMIA SERA ZA KINAZI

Instabul, Uturuki


RAIS Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amemshambulia Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel kwa kusema anatumia sera za kinazi.

Erdoğan ambaye mashambulizi yake yameripotiwa  na kituo cha luninga cha Uturuki, amemhoji Angela Merkel akisema. “Unatumia mbinu na sera za kinazi dhidi ya nani? Dhidi ya ndugu zangu Waturuki wanaoishi Ujerumani au ndugu zangu mawaziri waliokuja Ujerumani kushiriki katika maandamano yanayounga mkono mabadiliko ya katiba?,” alihoji.

Mvutano kati ya Uturuki na Ujerumani umeibuka katika siku za hivi karibuni baada ya Ujerumani kuwazuia mawaziri wa Uturuki kushiriki katika mkusanyiko wa waungaji mkono wa mabadiliko ya katiba yanayompa Rais Erdoğan wa Uturuki madaraka makubwa zaidi.

Ujerumani imewazuia baadhi ya mawaziri wa serikali ya Uturuki kushiriki katika mkusanyiko huo, suala ambalo limeikasirisha serikali ya Ankara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,885FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles