26.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 26, 2022

ERDOGAN ASHINDA KURA YA MAONI, WAPINZANI WAPINGA

ISTANBUL, UTURUKI


RAIS wa Uturuki, Recep Erdogan, ameibuka mshindi katika kura ya maoni ya kihistoria iliyofanyika juzi, ambayo inamwongezea mamlaka zaidi.

Matokeo hayo yameiacha nchi hiyo ikigawanyika na upinzani kulalamikia udanganyifu na umejipanga kuyapinga.

Mabadiliko  hayo  makubwa  ya  Katiba  yaliyoidhinishwa  kupitia kura hiyo yataongeza madaraka zaidi kwa Rais Erdogan  kuliko  kiongozi yeyote tangu  mwasisi  wa Taifa, Mustafa Kemal Ataturk  na mrithi wake Ismet Inonu.

Kambi  ya ‘ndio’ ilishinda  kwa  asilimia  51.4 ya  kura  dhidi  ya asilimia  48.6 ya ‘hapana’, Tume  ya  Uchaguzi ilisema  katika  taarifa zilizonukuliwa  na  shirika  la  habari  la Anadolu.

Wakati kura hizo zikitokana na asilimia 99.5 ya masanduku yaliyohesabiwa, mwitikio wa wapiga kura ulikuwa asilimia 85.

Lakini wapinzani katika  wilaya  zinazompinga Erdogan  za mjini hapa walionesha hasira kupinga matokeo hayo.

Mamia  ya  watu  pia  waliingia  mitaani  katika maeneo  ya  Besiktas  na  Kadikoy.

Kura  hiyo  ya  maoni  ilifanyika  chini  ya  amri  ya  hali  ya  hatari ambayo  imeshuhudia  watu  47,000 wakikamatwa  kufuatia jaribio  lililoshindwa  la  mapinduzi  dhidi  ya Erdogan Julai  mwaka  jana.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
176,803FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles