NA HERIETH FAUSTINE
MTAYARISHAJI wa muziki kutoka studio ya Sound Crafters, Enrico Figueroa ‘Enrico’, amesema nyimbo zote
zinazotoka siku hizi hazina ubora, ndiyo maana haziwezi kudumu hata kwa miaka miwili.
“Mpaka sasa sijaona wimbo mkali, nyimbo zote ni sawa tu, zinakaa siku mbili, tatu au wiki nne zinapotea, hakuna
Bongo Fleva ya kukaa miaka miwili,” alisema Enrico, alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha Planet Bongo
kinachorushwa na kituo cha runinga cha EATV.
Aliongeza kwamba ili wimbo uwe mkali na udumu muda mrefu, unatakiwa uwe na utungaji mzuri wenye mashairi bora na yenye vina vinavyoeleza uhalisia wa maisha ya sasa tofauti na nyimbo za siku hizi.