23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Endelezeni kielimu watoto wenye ulemavu – wito

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

MRATIBU Mkuu wa Mradi wa Elimu Jumuishi wa Kanisa la The Free Pentecostal Church Tanzania, Lucas Mhenga amewaomba wazazi,walezi na jamii inayoishi na watoto wenye ulemavu kutowaacha majumbani, badala yake waendelezwe kielimu ili waweze kufikia hatua ya vyuo vikuu. 

Ushauri huo,liutoa jijini hapa jana,  alipozungumza wakati wa kikao cha pamoja kilichowajumuisha kati ya wafanyakazi wa Jiji la Dodoma ,wazazi na walezi kwa ajili ya uanzishaji wa baraza la watoto wenye ulemavu Wilaya ya Dodoma Mjini. 

Alsema  ili wazazi na walezi wenye watoto hao waweze kujikomboa kupitia watoto wenye ulemavu wanatakiwa kuwasomesha kuanzia ngazi ya chini hadi chuo kikuu badala ya kuendelea kuwaweka majumbani huku wakiteseka kwa kukosa haki hiyo ya msingi ya kupata elimu. 

“Bado kuna ukatili,ubaguzi na manyanyaso kwa watoto wenye ulemavu majumbani walio wengi wamekosa elimu,matibabu na hata haki zao za kimsingi kama wanadamu wezao”alisema. 

Akizungumza kuhusu aunzishaji wa baraza hilo alisema limelenga kuwatambua watoto wenye ulemavu na kuwakutanisha ili wawe na sauti moja itakayowafanya kuzijua haki zao za msingi na wajibu.

Pia, kuwajengea uwezo wa mabaraza mengine ya watoto ulemavu katika kila ngazi husika ili yaweze kujumuika pamoja na mengine yawe chombo kimoja chenye nguvu na kudai na kutetea haki zao za msingi. 

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na Vijana Jiji la Dodoma, Sharifa Nabalang’anya,aliwataka  wazazi,walezi wenye watoto ambao wana ulemavu kutoona kama ni sehemu ya mkosi kwenye familia,wanachotakiwa ni kuhakikisha wanawaondolea kwa kuwaendeleza kielimu zaidi. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles