30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Emirates yaadhimisha miaka 25 ya huduma zake nchini Tanzania

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

KAMPUNI ya Ndege ya Emirates inaadhimisha miaka 25 ya huduma nchini Tanzania, kusaidia kuunganisha abiria na wafanyabiashara kutoka Dar es Salaam na duniani kote huku ikitaja mafanikio yake makubwa ya kukua kishughuli zake nchini.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mwishoni mwa wiki hii na Meneja wa Nchi wa Emirates nchini Tanzania, Abdullah Adnan alisema tangu mwaka 1997, Emirates imejivunia kuunganisha karibu wasafiri milioni 3 kwa zaidi ya safari 15,000 za ndege kati ya Tanzania hadi Dubai.

Amesema shirika lao la ndege limezidi kukua kishughuli nchini na kufanya kuwepo kuanza kwa  safari za  ndege mara moja kwa wiki inayoendeshwa na A310-300, kati ya Dubai na Dar es Salaam.

“Huduma za shirika hili letu zinazidi kukua  na kufikia hadi safari za kila siku zinazohudumiwa na shirika la ndege la Boeing 777-300ER, kulingana na mahitaji ya abiria na mizigo,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo na kuongeza: 

“Miaka miwili iliyopita imekuwa migumu kwa watu wengi na viwanda, lakini Kampuni hiyo ya Emirates imekuwa ikifanya kazi kwa bidii ili kujenga upya mtandao wake kwa usalama huku ikiweka kipaumbele kwa wateja wake, wafanyakazi, na jumuiya inazohudumia duniani kote,” ameeleza.

Amesema walipaa angani na kufika Tanzania kwa mara ya kwanza miaka 25 iliyopita, wakiwa na dhamira ya kuunganisha wasafiri wa Tanzania na duniani kote, na kuwapa uzoefu ambao uliendana na  mahitaji yao.

“Tunajivunia hatua hii muhimu, na tuna heshima kubwa kuitumikia Tanzania kusaidia kuleta familia pamoja, kusafirisha watalii kwa ndege katika nchi hii nzuri na kuonyesha vivutio vyake, na kusaidia kuongeza nguvu za uchumi wake,” alisema na kuongeza:

“Tunajivunia kwamba tumeweza kuimarisha uchumi kupitia shughuli zetu za SkyCargo, na tunapanga kuendeleza dhamira yetu ya kutumikia Tanzania kupitia uzoefu wa hali ya juu wa usafiri wa anga na kwa kusaidia jamii na uchumi wa ndani,” amesema.

Amesema Emirates SkyCargo imekuwa ikisaidia uchumi wa Tanzania kwa kuwezesha mauzo ya nje kwenda duniani kote. Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, Emirates SkyCargo, imebeba zaidi ya tani 660,000 kwenda na kurudi Tanzania.

Mizigo ya nje ya Dar Es Salaam mara kwa mara inajumuisha vitu vinavyohitaji uhifadhi wa makini kama vile nyama ya mbuzi na kondoo, samaki kaa, kamba na parachichi. SkyCargo pia inasaidia kuagiza sehemu za mashine pamoja na vifaa vya elektroniki nchini.

Emirates SkyCargo pia ilikuwa nguzo ya nguvu kwa jamii ya wenyeji wakati wa janga la kiafya kwa kusafirisha na kutoa vifaa muhimu vya matibabu na chanjo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles