30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Emirates kutekeleza mradi mkubwa zaidi wa ukarabati wa ndege zake

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Shirika la Ndege la Emirates imeanza mipango yake ya kuboresha madaraja yote ya ndani ya ndege zake 120 aina ya Airbus A380 na Boeing 777 huku mbili zikiwa ni kati ya ndege kubwa zaidi za kibiashara zinazohudumu hivi sasa.

Mradi huo kabambe unaowakilisha uwekezaji wa mabilioni ya dola unalenga kuhakikisha kuwa wateja wa Emirates wanasafiri vizuri kwa miaka ijayo.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Mapema wiki hii na Shirika hilo la Emirate imeeleza kuwa mradi huo utaanza rasmi Novemba, mwaka huu ukisimamiwa kikamilifu na timu ya Uhandisi ya Emirates.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa lengo la kufanya mradi huo ni kurudisha ndege nne za Emirates kuanzia mwanzo hadi mwisho kila mwezi, mfululizo kwa zaidi ya miaka miwili. 

”Ndege zitakazokarabatiwa upya na kurudi katika huduma, 53 ni aina ya 777s ambazo zitarekebishwa, viti 4,000 vya Premium Economy vitafanyiwa ukarabati na kurudishwa katika hali ya upya, sehemu 728 za Daraja la kwanza zitarekerekebishwa na zaidi ya viti 5,000 vya Daraja la Biashara kuboreshwa hadi kuwa na muundo na mtindo mpya mradi utakapokamilika mwezi wa Aprili 2025,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Mbali na ukarabati huo pia  mazulia na ngazi zitaboreshwa na sehemu za ndani zitakuwa na muonekano mpya pamoja na kupakwa rangi upya na mchoro wa mti wa ghafi ambao asili yake ni UAE.

”Hakuna shirika lingine la ndege ambalo limeshughulikia ukarabati wa ukubwa huu ndani ya ndege, na wala ubunifu wa michoro kama hiyo, hivyo timu za Uhandisi za Emirates zimekuwa zikipanga na kufanya majaribio kwa mapana, ili kuanzisha na kurahisisha michakato, na kutambua na kushughulikia changamoto zozote zinazoweza kutokea,” ilieleza taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles