32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Emery kuachiwa timu hadi Januari

LONDON, ENGLAND

UONGOZI wa timu ya Arsenal, umeweka wazi kuwa, unamuachia Unai Emery kikosi hicho hadi Januari mwakani aweze kubadilisha mwenendo, lakini akishindwa kufanya hivyo itakuwa mwisho wa kibarua chake.

Kwa sasa uongozi huo unaamini Emery ni kocha sahihi ambaye anaweza akabadilisha matokeo hasa kwa kipindi hicho ambacho amepewa japokuwa mashabiki wameanza kutembea na mabango ya kumtaka kocha huyo kuondoka.

Washinda bunduki hao wa jijini London, wameshinda michezo miwili katika michezo 10 iliopita ya Ligi Kuu England, lakini wanashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi baada ya kucheza michezo 12 na kujinyakulia pointi 17.

Mmiliki wa timu hiyo Raul Sanllehi na Mkurugenzi wa michezo wa Vinai Venkatesham, juzi walikutana na uongozi wa timu kwa ujumla na kuweka wazi kuwa hawafurahishwi na matokeo ya sasa ya Arsenal, lakini wanatakiwa kumuamini kocha huyo hadi Januari mwakani.

“Tunasikitishwa na matokeo tunayoyapata kwa sasa pamoja na haina ya uchezaji wa timu kwa ujumla. Tunaungana na mashabiki, kocha, wachezaji kwa kuwa sio mwenendo ambao tulikuwa tunautarajia.

“Lazima mambo yabadilike ili kwenda sawa na matakwa ya timu msimu huu, hivyo tunaamini Emery ni kocha sahihi wa kubadilisha mwenendo wa timu hii, kwa pamoja tunatakiwa kumuunga mkono, tunaamini kwa kufanya hivyo kila kitu kitakuwa sawa,” walisema uongozi wa timu hiyo kwenye kurasa za mitandao ya kijamii.

Awali kulikuwa na taarifa kwamba kocha huyo anaweza kufukuzwa kazi muda wowote kutokana na mwenendo wao, hivyo kumekuwa na baadhi ya makocha wakitajwa kuja kuchukua nafasi hiyo.

Miongoni mwa makocha ambao wanatajwa wanaweza kuziba vizuri nafasi hiyo ni pamoja na aliyewahi kuwa kocha wa Barcelona, Luis Enrique, Jose Mourinho pamoja na kocha msaidizi wa timu ya Manchester City, Mikel Arteta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles