22.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

ELIMU YA MZAZI HAINA MSAADA KATIKA MALEZI

77137460-1

WATU wengi hufikiri kuwa kiwango cha elimu anachokuwa nacho mzazi kinachangia katika malezi bora ya mtoto.

Wapo wazazi ambao wanakata tamaa kabisa  ya watoto wao kufika mbali kielimu kutokana na mazingira ya nyumbani kwake pamoja na elimu ndogo aliyonayo.

Kuna baadhi ya watu wanadhani saikolojia na uelewa unahusishwa  na elimu ya mzazi, jambo ambalo si kweli.

Tafiti zilizofanywa katika nchi mbalimbali za Afrika zinaonyesha kwamba, hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya elimu, kipato wala mafanikio ya kimaisha ya wazazi na ubora wa malezi ya watoto wao.

Hali hii inajionyesha baada ya kuonekana wazazi wasio na elimu na wenye kazi zisizo na hadhi ndio wanaoonekana kuwajibika zaidi katika masuala ya ufuatilia wa makuzi ya mtoto kuliko wenzao wenye elimu ya kuanzia shahada na kuendelea.

Tafiti hizo pia zinaonesha wazazi wenye elimu kubwa hawapati/hawana muda wa kukaa na kuwasiliana na watoto wao ipasavyo.

Kinachofanywa na wazazi wenye kipato ni kuweka mazingira mazuri ya kujifunzia nyumbani, ikiwamo vitabu, televisheni  na vifaa vingine.

Kwa upande mwingine, wazazi wasio na elimu wala kazi zenye hadhi, wameonekana kuwa na uhusiano na watoto, wakitumia muda mwingi kuwafunza watoto tabia zinazokubalika katika jamii zao.

Hata hivyo, wazazi hawa wameonekana kushindwa kuweka mazingira rafiki ya kujifunzia maisha majumbani kwao kama wenzao wenye elimu.

Kundi hili la watu wasio na elimu baadhi yao huwa wanakuwa na malezi bora kwa watoto kwakuwa wanakuwa wakiishi kwa kuwasikiliza pamoja na kuwapa njia ya kutatua changamoto mbalimbali  katika jamii.

Wazazi wenye elimu mara nyingi hulelewa watoto wao na wadada wa kazi ama ndugu ambao kama hawana nia nzuri wanachangia kuwaharibu kitabia.

Unakuta mzazi anatumia muda mwingi kufanya kazi za ofisi na kurudi nyumbani jioni wakati mwingine usiku kabisa na kukuta mtoto ameshalala, hivyo si rahisi kujua amekumbana na matatizo gani mchana.

Wazazi tunapaswa kuwa makini sana katika malezi kwa kutenge muda maalumuy wa kukaa na watoto na kuwasikiliza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles