30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 9, 2021

Elimu ya kodi kuingizwa kwenye mitaala

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imesema ipo katika mchakato wa kuweka elimu ya kodi katika mitaala (syllabus) ya elimu nchini ili wanafunzi waanze kufundishwa maana ya kodi tangu wakiwa wadogo.

Hatua hiyo inatokana na kuwapo kwa uelewa mdogo katika masuala ya kodi ambao unachangia kwa kiasi kikubwa wafanyabiashara wengi hasa wanaoanzisha biashara kuona ulipaji kodi ni mzigo.

Akizungumza katika mafunzo ya kodi kwa wafanyabiashara wadogo na wakati, Ofisa Elimu Mkuu kwa Mlipakodi kutoka TRA, Rose Mahendeka amesema mchakato huo unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya The Tanzanian Associate kwa kushirikiana na Kampuni ya Abel and Fernandes Communications, yalilenga kuwakuelimisha jamii kuhusu masuala ya kodi.

Aidha, Mahendeka alisema bado kuna changamoto ya baadhi ya wafanyabiashara kutoelewa umuhimu wa kulipa kodi pamoja na kuweka kumbukumbu za mapato na matumizi katika biashara zao.

“Wafanyabiashara wengi hawana uelewa wa kodi ila tupo katika mchakato wa kuweka elimu ya kodi katika mitaala ya elimu waanze kupata wakiwa wadogo kabisa kule mashule ili waanze kupata uelewa wakiwa wadogo kabisa  kwamba nini maana ya kodi, inahusu nini na jinsi gani kodi inalipwa Tanzania, tunaamini kwa njia hiyo watu wengi wataelewa,” amesema.

Naye Mshauri wa masuala ya Kodi, Petro Francis alisema ni muhimu sana kwa wafanyabiashara wa ngazi zote kuelewa maana ya kodi na umuhimu wa kulipa kodi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,702FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles