25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Elimu ya afya ya uzazi inahitajika kwa watu wenye ulemavu-Songambele

Na Upendo Mosha, Moshi

Jamii ya watu wanaoishi na Ulemavu hususan Wanawake na Vijana wametajwa kuwa katika hatari kubwa ya kuambukizwa virusi vya ukimwi na magonjwa ya ngono kutokana kukosa haki ya kupata elimu ya afya ya uzazi na makuzi.

Hayo yamebainishwa Leo Mei 27, 2021 na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilokuwa la kiserikali linalojishughulisha na ulemavu kwa wanawake na watoto la Songambele, Faustina Urassa, wakati wa semina ya utoaji elimu ya uzazi na makuzi kwa watu wenye ulemavu, Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Amesema haki za binadamu ni pamoja na walemavu kupata elimu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi pamoja na magonjwa ya ngono lakini jambo hilo limekuwa tofauti kutokana na jamii kutowashirikisha katika elimu hizo na kuwa kwenye hatari zaidi ya kukumbwa na magonjwa haya hatari.

“Watu wenye ulemavu wapo katika hatari kubwa zaidi ya kuambukizwa kirahisi virusi vya ukimwi pamoja na magonjwa ya ngono maana jamii imewatenga na wameoneka wao hawafai…wanasahau kuwa mtu mwenye ulemavu anahaki zote maana na yeye anahisia za kimapenzi kama mtu mwingine yeyote,” amesema Urassa.

Amesema elimu ya afya ya uzazi imekuwa ni changamoto kubwa kwa walemavu jambo ambalo limekuwa likisababisha baadhi ya kupata mimba zisizotarajiwa pamoja na kuambukizwa magonjwa mbalimbali ikiwemo ukimwi na kukatisha ndoto zao.

Mbali na hilo Urassa amesema changamoto nyingine inayowakabili wanawake wenye ulemavu ni kushindwa kumudu gharama za manunuzi ya taulo za kujisiti wakati wa hedhi jambo ambalo limekuwa kujidhalilisha utu wao.

“Walemavu kutokana na kukaa muda mrefu taulo hizi za kawaida hazitusaidi hivyo tumekuwa tukitumia pampas za watu wazima ambazo ni ghali sana kwa siku si chini ya elfu 6000 wengi hawawezi na ikifika kipindi cha hedhi wanapata tabu ambayo inadhalilisha utu wake,” amesema Urassa.

Amesema kutokana na hali hiyo ameiomba serikali kutoa kodi katika taulo hizi jambo ambalo litasaidia kushusha gharama na kuwasaidia walemavu kujistiri wakati wa hedhi.

Naye Meneja mradi wa shirika hilo, Abud Munisi, ametoa wito kwa jamii hususan wanaume kushiriki vema katika makuzi ya watoto na kuacha tabia ya kuona jukumu hilo ni la mzazi wa kike kwani ni jukumu la malezi ni la jamii nzima na sio la mwanamke pekee.

Jolieth Poul ambaye anaishi na ulemavu amesema mafunzo hayo yatawasaidia kutambua njia kujikinga na maambukizi ya magonjwa mbalimbali ya ngono na kwamba jamii inawajibu wa kutahamini walemavu na kuwapa haki sawa na watunwengine ikiwemo elimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles