Eli Pascal awaweka tayari mashabiki

0
231

NASHVILLE, MAREKANI

MWIMBAJI na mtunzi wa nyimbo za Injili nchini Marekani, Eli Pascal, amewaweka tayari mashabiki kwa video ya wimbo wake mpya utakaotoka hivi karibuni mtandaoni.

Akizungumza na MTANZANIA , Pascal ambaye amewahi kutamba na nyimbo, Kesho Yangu na Zero To Hero, alisema anaamini wimbo huo utagusa maisha ya watu kutokana na ujumbe wake.

“Mashabiki wake tayari, nipo ‘location’ namalizia video yangu mpya, ni wimbo mzuri uliobeba ujumbe ambao utamgusa kila mmoja, hivyo watu wakae tayari kuipokea video hii,” alisema Eli Pascal.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here