Efm radio wakutanisha ‘wanawake wa shoka’

0
757

1-11NA ASIFIWE GEORGE

KATIKA kuadhimisha Siku ya Wanawake duniani kituo cha redio cha EFM kimekutanisha wanawake kutoka vikundi mbalimbali vya ujasiriamali na Vicoba kutoka Jiji la Dar es Salaam na Pwani kwa lengo la kuwapatia elimu ya ujasiriamali.

Rais wa vikoba Tanzania, Devotha Likokola ambaye alipewa tuzo ya ujasiriamali, alisema lengo lingine la kukutanisha wanawake hao ni kuelezana changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake katika biashara zao na maisha kwa ujumla.

Likokola aliwahimiza wanawake kuwa na uthubutu na kuwasihi wakina mama wasikate tamaa katika kujishuhulisha na biashara mbalimbali ili waweze kujikimu kimaisha.

Meneja wa mafunzo, Anna Manoti kutoka TECC, aliwaelimisha wakinamama kwa kutumia dhana ya ujasiriamali ikiwemo kujitambua, kufahamu kitu ambacho unataka kukifanya na kujua jamii inayokuzunguka inaweza kukusaidiaje katika kuendeleza biashara yako.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here