24.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 29, 2023

Contact us: [email protected]

Edmund aipeleka GB nusu fainali Davis Cup

Kyle Edmund
Kyle Edmund

BELGRADE, SERBIA

NYOTA wa tenisi wa timu ya Great Britain, Kyle Edmund, amefanikiwa kuipeleka timu hiyo hatua ya nusu fainali katika michuano ya Davis Cup, baada ya kumchapa mpinzani wake, Dusan Lajovic wa timu ya Serbia.

Edmund alishinda hatua hiyo katika seti ya tatu ambapo mchezo huo ulimalizika huku Great Britain ikishinda kwa seti 6-3, 6-4 (7/5), hivyo kumfanya bingwa wa michuano ya Wimbledon, Andy Murray kuwa na furaha kubwa.

Awali, Murray alitolewa kwenye michuano hiyo, hivyo Edmund akabaki kuiwakilisha timu hiyo na kuifanya ifike nusu fainali, hata hivyo Murray anaamini kuna uwezekano mkubwa wa kutwaa ubingwa.

“Ukiwa nje ya uwanja unaona makosa mengi ya mwenzako, nilikuwa najisikia vibaya baada ya kuona mchezaji mwenzangu, Edmund akifanya baadhi ya makosa, lakini kwa pamoja tunashukuru kuweza kuingia hatua ya nusu fainali.

“Tunaamini tuna nafasi ya kuweza kusonga mbele katika michuano hii ya Davis Cup na kuweza kutetea ubingwa, tupo tayari kuleta furaha kwa taifa letu, hivyo mashabiki waendelee kutuunga mkono,” alisema Murray.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,750FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles