25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Eddy Kenzo, Khaligraph wampiga tafu Lulu Diva

Jessca Nangawe

WAKATI mwanadada Lulu Diva akitarajia kuachia albamu yake mpya mapema mwezi huu, mastaa wakubwa kutoka Afrika Mashariki wamempiga tafu kunogesha albamu hiyo.

Lulu Diva alisema anatarajia kauchia albamu yake mapema mwezi huu ambapo itakuwa ya kwanza tangu aanze muziki inayojulikana kwa jina la The 4 Some ikiwa na nyimbo 18.

Alisema ndani ya albamu hiyo wapo wasanii wakubwa kama EddyKenzo wa Uganda, rapa kutoka nchini Kenya, Khaligraph Jones pamoja na Fid Q kutoka Tanzania.

“Ni albamu ambayo inabeba mambo mengi kuhusu fedha, mapenzi na mafanikio, natarajia itakua ya kitofauti na wasanii wengine, kikubwa mashabiki zangu watakutana na surprise nyingine lakini pia wapo wasanii wengine kutoka ukanda huu wa Afrika Mashariki,” alisema mrembo huyo.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles