29.8 C
Dar es Salaam
Monday, October 7, 2024

Contact us: [email protected]

ED SHEERAN ATIKISA UINGEREZA

LONDON, ENGLAND


STAA wa muziki nchini England, Edward Christopher maarufu kwa jina la Ed Sheeran, ametikisa nchini humo baada ya kutajwa kuwa namba moja kwa wasanii walioingiza fedha nyingi mwaka huu.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye anatamba na wimbo wake wa ‘Thinking Out Loud’ ametajwa kuwa mwaka huu ameingiza kiasi cha pauni milioni 80 na kuwa msanii wa kwanza nchini humo kuingiza kiasi hicho cha fedha.

Hata hivyo, mbali na kuonekana kuwa namba moja mwaka huu, lakini hajaweza kufikia rekodi iliyowekwa na staa wa muziki nchini humo Adele, ambaye aliweka historia ya kuingiza kiasi cha pauni milioni 140 kwa mwaka.

Wimbo wa Thinking Out Loud, ambao upo kwenye albamu ya msanii huyo ambayo iliachiwa tangu 2014, umezidi kumpa jina msanii huyo pamoja na shoo kwenye matamasha mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles