Mwandishi wetu,
Benki ya Ecobank imesainiwa rasmi kuingia kwenye kanuni sita za Umoja wa Mataifa za benki zinazowajibika ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kukuza mazingira ya ukuaji wa benki hiyo kupitia ushirikiano wa ubunifu kati ya benki duniani na Mpango wa Programu ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa (UNEP FI).
Kanuni hizo zilizoundwa na Wajumbe wa UNEP FI, zinalinganisha sekta ya benki na malengo ya maendeleo ndelevu ya umoja wa mataifa na makubaliano ya hali ya hewa yaliyofanyika mjini Paris mwaka 2015.
Akizungumza baada ya kusainiwa katika mpango huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank, Ade Ayeyemi amesema wanayachukulia majukumu yao kwa umakini kwa kuhakikisha kuwa majaribio ni muhimu katika kipindi cha kufanya maamuzi, uongozi, shughuli za biashara na shirika kwa ujumla.
“Pamoja na umakini wetu kwa wateja wetu na dhamira ya kuwa mshauri anayeaminika, tunatumia cheo chetu cha uongozi katika kufanya maamuzi na hatua zetu kwa kuzingatia malengo ya jamii na vizazi vijavyo vya Afrika.
“Kwa kujiunga na kanuni sita za benki zinazowajibika tunautangazia umma kwamba tutafuata na kudumisha viwango ambayo yamepitishwa na benki kubwa duniani,” amesema Ayeyemi.
Lengo kuu la kanuni hizo ni kuunda sekta ya kifedha ambayo itasaidia watu na dunia kwa ujumla huku ikitoa matokeo mazuri na kuboresha maisha ya watu, bila kuathiri vizazi vijavyo pia huongoza benki katika uwakilishi wao na kuwapa changamoto zinazowasaidia kuongeza mchango wao katika jamii kwa ajili ya maisha ya baadaye.
Ecobank imesainiwa kwenye UNEP FI tangu mwaka 2009 na hadi sasa mpango huo una wanachama 274 kutoka kwenye taasisi za kifedha, viwanda, bima na uwekezaji.