32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Ebola tishio DRC


KINSHASA, DRC

TAKRIBANI watu 1,000 wametangazwa kufariki dunia kutokana na ugonjwa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kuzua wasiwasi wa kusambaa zaidi ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Afya ya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, idadi ya watu waliofariki inaweza kuongezeka kutokana na wasiwasi kuwa huenda watu wakazidi kuambukizwa siku zijazo.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema hali mbaya ya usalama, uhaba wa fedha na kauli za wanasiasa zinazowachonganisha wahudumu wa afya na raia zimeathiri kwa kiasi kikubwa juhudi za kupambana na ugonjwa huo.

Wakati huo, Mkurugenzi Mtendaji wa kitengo cha dharura cha Shirika la Afya, Michael Ryan ametahadharisha kwamba maambukizi ya ugonjwa wa Ebola yataendelea.

Ryan amesema chanjo dhidi ya ugonjwa huo zipo, lakini hazitoshi na kwamba zaidi ya watu 110,000 wameshapewa chanjo tangu kulipuka kwa maradhi hayo. Nchi jirani za Rwanda na Uganda pia zinaendelea na zoezi la kuwachanja wahudumu wake wa afya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles