27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

EACJ kuamua rufani ya Komu Novemba

Antony Komu
Antony Komu

 Na JANETH MUSHI,  ARUSHA

MAHAKAMA ya Haki ya Afrika Mashariki (EACJ), inatarajia kutoa hukumu iliyofunguliwa na Serikali ya Tanzania Novemba mwaka huu, dhidi ya Antony Komu ambaye alishinda kesi aliyofungua dhidi ya Bunge la Tanzania.

Katika kesi hiyo, Komu ambaye ni Mbunge wa Moshi Vijijini (Chadema), alidai kuwa Bunge hilo limekiuka ibara ya 50 ya Mkataba wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa kukiuka uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Aprili 17, mwaka 2012 na kuiomba mahakama hiyo  kutoa tafsiri ya kisheria.

Kesi hiyo ilikuwa inasikilizwa na jopo la majaji watano wakiongozwa na Rais wa jopo hilo, Jaji Dk. Emmanuel Ugirashebuja, Makamu wake Libore Nkurunzinza, Edward Rutakangwa, Aaron Ringera na Geoffrey Kyiryabwirwe.

Jaji huyo aliwaagiza mawakili wa upande wa Serikali ya Tanzania kuwasilisha hoja zao kimaandishi ndani ya siku 14 kuanzia jana na upande wa wajibu rufaa (Komu), kujibu hoja hizo ndani ya siku 14.

Katika uchaguzi huo Komu alikuwa mgombea pekee wa nafasi ya ubunge wa EALA, kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Awali Wakili Mkuu Mwandamizi wa Serikali, Mark Mulwambo akisaidiana na Pauline Mdendemi walipinga na kudai mahakama hiyo ya EACJ haina uwezo kisheria wa kutoa uamuzi kuhusu Bunge ambalo ni mwanachama wa EAC.

Mawakili wa Utetezi Edson Mbogoro na John Mallya, walidai mahakama hiyo ina uwezo wa kutoa tafsiri ya kanuni za uchaguzi wa wabunge wa EALA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles