27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 16, 2024

Contact us: [email protected]

EAC YAKABILIWA NA UHABA WA FEDHA

KAMPALA, UGANDA

MATAIFA ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanahitaji kiasi cha Dola za Marekani bilioni 78 kufanikisha miradi mbalimbali ya miundombinu kwa lengo la kuimarisha uchumi katika Jumuiya hiyo.

Viongozi wa Jumuiya hiyo wamekutana jijini Kampala, nchini Uganda na wamekubaliana kuwa Dola bilioni 62 zitatengewa ujenzi wa reli ya kati, barabara na mradi wa nguvu za umeme.

Kilomita 7,600 za barabara, reli ya kati kilomita 4,000 na Megawati 6,734 zinatarajiwa kujengwa katika mataifa yote sita ya Jumuiya hiyo. Kukamilika kwa miradi hiyo kutasaidia pia kurahisisha usafiri wa watu na bidhaa pamoja na kuinua uzalishaji wa bidhaa.

Miradi ya afya pia inatarajiwa kuimarishwa, ikiwa ni pamoja na kujenga taasisi za afya, utafiti na dawa kwa lengo la kuwasaidia wakazi wa nchi za Afrika Mashariki.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa, kati ya Dola bilioni 78 za Marekani, ni Dola bilioni 5 ndizo zilizopatikana kuanza kwa miradi hii. Jumuiya hiyo inatarajia ufadhili kutoka Mataifa ya Ulaya kufanikisha miradi hiyo. Miradi hii inatarajiwa kumalizika kufikia mwaka 2025.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles