DUUH! SASA MADEMU WANALAZIMISHA NDOA KITAA

0
902

Na RAMADHANI MASENGA

OIOIOI majita! Mko poa? Mambo yanakwenda? Aisee mlume niko poa na ngoma naikimbiza ile mbaya mbali na changamoto kadhaa ambazo zinaleta shobo katika reli.

Laifu bila changamoto ni la wapi hilo? Hakuna. Changamoto katika maisha ni kama pilipili katika chakula. Inatia ladha fulani hivi.

Ila wanangu mnawasoma mademu siku hizi? Ukikutana na demu na kupiga naye stori mbili tatu tu lazima akuulize kama umeoa. Na kama ukimwambia hujaoa, fasta atakuambia hata yeye hajaolewa kisha ataanza shobo. Hahaha hatari sana.

Nakumbuka kitambo. Kila demu ukimtongoza, mbali na kukuzingua kinoma ila suala la kuolewa walikuwa wanaleta mizinguzi kinoma. Kwanza utawaza hata kumuona kwa namna anavyojiweka wa juu?

Ukitoka naye tu, hivyo vinjwaji, hayo matumizi, hata kama ulitaka kumuoa nyongo inaingia ndani. Mambo yako sasa hivi. Hata demu ukimpa buku tatu anashukuru kana kwamba umenusuru maisha yake kwa kumtolea figo. Hahaha maisha matamu sana nyakati hizi.

Kuna wakati huwa naogopa hata kumtokea jombo. Maana ukiongea nalo kidogo tu na kutupia ndoano zako, kesho mapema tu utaliona liko ghetto. Na ukiwa sio kauzu, deile atakuwa anakuja na kuacha nguo zake moja moja. Kufumba na kufumbua unakuta tayari kahamia mjengoni.

Ama kweli kutesa kwa zamu. Zamani tulibembeza kuwaoa, sasa hivi wanatubembeza kuwaoa. Anko Magu kamba uliyoshika usiiachie heshima mtaani ipatikane.

Majita.. mademu sasa wanadisplini kinoma. Hawana mbwembwe wala matusi kwa majita. Sasa hivi bila kujali unapiga mzigo wapi unang’oa demu mkali kinoma halafu kiulaaaini.

Akuringine, kisha pesa ya vocha apewe na nani? Pesa ya bajaji aiokote wapi? Wale mafaza waliokuwa wanawapa jeuri mjini, ngoma ngumu baada ya pesa za dili kupigwa pini.

Sasa wahongwe na nani? Hata wale wachache waliokuwa wameajiriwa katika maofisi kwa sababu ya uzuri wa maumbo na sura zao na sio taaluma wamepigwa chini. Hawana vyeti, kama wanavyo ni feki.

Kwa hali hii unadhani mtaani kutakosa heshima? Acheni mwana nitambe. Zamani nimepigwa sana vibuti aisee. Vihela vyangu vya ngama vilikuwa vinaonekana kama takataka. Ila sasa, naishi kama milionea vile.

Katika simu yangu nina orodha ya mademu kama saba na wote wanataka ndoa na mimi. Hahaha, eti wanaamini mimi kachaa naweza kuwaoa kipindi hiki. Hivi hapa Dar hakuna branch ya milembe kweli?

Maana nahisi watakuwa wamedata. Niwaoe sasa, halafu baadaye mihela ikianza kumwagika si wataninyanyapaa kama kitambo hawa?

Uzuri wa mademu wa Kibongo wanapenda sana maisha ya kuigiza. Sasa kwa kuwa mlume mjini kitambo, basi na mimi nakuwa dairekta wao tu. Mbona wananikoma.

Ukijifanya Sharukh Khan kwa mademu hawa wa Kibongo unakufa kwa presha bure. Demu mmoja lakini katika simu yake kuna honey, babe, sweet, hubby, my world na uchafu mwingine kibao.

Ukiingia kichwakichwa mademu wa namna hii si utakufa kwa presha? Yanini sasa.

Ila wanangu mbali na yote inabidi mcheze fea. Mademu wa mjini wana upupu, usipokuwa makini lazima ukuwashe! Najua mmenisoma wanangu. Kama vipi next time.

Ni mimi mwanenu wa nyakati zote. Nasepa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here