30.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

DURTETE: NITAWATUPA MAFISANI KUTOKA KATIKA NDEGE ANGANI

MANILA, PHILIPPINES


rodrigo-duterteRAIS wa Philippine, Rodrigo Duterte, ametishia kuwarusha viongozi mafisadi kutoka katika ndege angani, akisema ameshawahi kufanya hivyo kitambo.

Duterte aliyasema hayo Jumanne wiki hii wakati akiwahutubia waathirika wa kimbunga katikati ya Philippines.

“Kama wewe ni fisadi, nitakubeba kwa kutumia helikopta hadi Manila na kukurusha nje,” alisema Duterte, ambaye ameanzisha vita dhidi ya ufisadi na mihadarati.

Alitishia kutoa adhabu hiyo kwa yeyote atakayeiba fedha za msaada alizoahidi kuzitoa.

“Nimefanya hivi kitambo, kwanini nisiweze kufanya tena?” alisema huku akishangiliwa na watu hao.

Haya ni madai mapya ya rais huyo ambaye amekiri kutekeleza mauaji ya kiholela.

Hata hivyo, msemaji wake amepinga madai hayo.

Mapema mwezi huu, msemaji mwingine, Martin Andanar, alisema kauli za mwajiri wake zipokewe kwa makini, lakini zisipewe uzito baada ya kusema kuwa aliwaua watu watatu alipokuwa Meya wa Davao nchini humo.

Wakati kauli hiyo mpya akiitoa Jumanne wiki hii, jana Rais Duterte alionekana kujiweka kando na kauli zake za awali.

“Helikopta, nimtupe mtu? Na iwapo ni kweli, sitakiri,” alisema wakati wa mahojiano na shirika la habari la ABS-CBN.

Rais huyo ana historia ya kuyakana maneno yake.

Watu 6,000 wanasemekana kuuawa na polisi, wanamgambo na wauaji wa kukodi nchini hapa tangu Duterte azindue vita dhidi ya mihadarati baada ya kuchaguliwa kuwa rais Mei, mwaka huu.

Wanasiasa wa upinzani na makundi ya haki za binadamu wamekuwa wakitaka aondolewe madarakani, lakini amebakia maarufu miongoni mwa wapigakura wanaotaka aisafishe nchi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles