24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Dunia imebadilika hatuwezi kubaki na sheria hizi za habari-Silaa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzana Digital

Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa ameahidi kushirikiana na wabunge wenzake katika kuhakikisha tasnia ya habari inakuwa na sheria rafiki zinazotekelezeka.

Silaa ametoa kauli hiyo leo Jumatano Novemba Novemba 8, 2022, wakati akizungumza na uongozi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Wadau wa Haki ya Kupata Habari (CoRI), jijini Dodoma.

TEF na CoRI wamekutana na mbunge huyo kuzungumzia baadhi ya vipengele vilivyopo kwenye sheria ya habari ya mwaka 2016 vinavyokandamiza uhuru wa habari nchini.

‘‘Mimi na wabunge wenzangu tutashirikiana. Dunia imebadilika na hatuwezi kubaki hapa tulipo,” amesema Silaha na kuongeza kuwa: “Nitazungumza na wenzange na kisha tutaona namna ya kufanya,’’.

Kikao hicho nje ya viwanja vya bunge, kiliongozwa na Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile, ambpo alimweleza mbunge Silaa kwamba, sheria ya habari ya mwaka 2016 imeweka mazingira makubwa ya kumuhofisha mwandishi wa habari.

Aidha, amesema kuwa ndani ya sheria hiyo kuna vipengele mbalimbali kwa undani wake ambavyo vinaua tasnia ya habari akitolea mfano kipengele kinachompa nguvu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo kufungia chombo cha habari kwa namna anavyoona inafaa.

‘‘Katika safari ya mabadiliko haya, tumeungana taasisi zote za habari ili kuwa na kauli moja. Tumeunganisha nguvu ili kufikia lengo,” amesema Balile.

James Marenga, Mjumbe wa CoRI kutoka Taasisi ya Vyombo ya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania alimweleza mbunge Silaa kwamba, tasnia ya habari haina tifauti na tasnia nyingine nchini katia utendaji kazi.

Wakili Marenga amabaye ni wakili wa kujitegemea alisema, ikiwa mawakili wanatengeneza taratibu zao na kuzifanya kuwa rejea katika kazi zao, inashindikanaje wanahabari nao wakajiwekea utaratibu wa ‘kujihukumu’ kama ilivyo tasnia nyingine?

‘‘Mimi ni mwanasheria, katika taasisi yetu tulitengeneza cord of conduct wenyewe na hizo ndio zinatuongozi, ni busara na wanahabari wakawa na utaratibu wao kisheria unaosimamiwa na wenyewe katika kuhakikisha maadili ya uandishi wa habari yanafuatwa,’’ amesema Wakili Marenga.

Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Media Brains Inc Ltd, Jessy Kwayu amesema sheria ya habari ya mwaka 2016 ilipitishwa katia mazingira ambayo si rafiki.

‘‘Vipengele 19 vya sheria hiyo vilijaribiwa kwenye sheria za nchi, vikaonekana kutoingia katika mizani ya kisheria,’’ amesema Kwayu.

Rose Reuben, Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA, amesema kwa mazingira ya sasa, waandishi wanashindwa kuandika habari kwa uhuru.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles