31.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, January 31, 2023

Contact us: [email protected]

DUKA LA DAWA LAGEUZWA HOSPITALI YA KUNG’OA MENO


NA EDITHA KARLO

KIGOMA


MMILIKI wa duka la dawa katika eneo la Kibirizi  Manispaa ya Kigoma Ujiji ametiwa mbaroni na polisi kwa tuhuma za  kuendesha duka  la dawa kama Hospitali huku akitoa huduma mbali mbali ikiwamo kung'oa meno.

Mmiliki huyo amekamatwa baada ya ukaguzi uliofanywa na timu ya idara ya afya ya Halmashauri ya Manispaa ya kigoma Ujiji ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo, Dk. Peter Nsanya.

Dk. Nsanya amesema katika ukaguzi wao wamegundua kwamba pamoja na kuendesha shughuli mbalimbali zikiwemo za uuzaji wa dawa, kuchoma sindano, kung’oa meno na mambo mengi ya matibabu ya afya huku akiwa hana kibali cha kuendesha shughuli hiyo lakini pia akiwa hana vyeti vya kitaaluma vya kutoa huduma hizo.

Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Hussein Ruhava amewataka wakazi wa maeneo jirani na duka hilo kutumia vituo vya afya na zahanati zilizo rasmi na hasa zile za serikali ambazo zina uhakika na uendeshaji wake kwa ajili ya kulinda afya zao. 

Hata hivyo, tofauti na ilivyotegemewa na wengi wananchi wa eneo hilo wameeleza kusikitishwa kukamatwa kwa mmiliki huyo na kufungwa kwa duka hilo ambalo wanasema kuwa lilikuwa tegemeo lao kubwa katika kupata tiba kwa haraka.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles