26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Duka la dawa Bagamoyo lasaidia wananchi

Na MWANDISHI WETU-BAGAMOYO

DUKA la dawa linalomilikiwa na Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, limetajwa kuwa mkombozi wa upatikanaji wa huduma kwa wananchi wanaofika hospitalini hapo.

Kutokana na hali hiyo, kwa sasa hali ya upatikanaji dawa  imekuwa ni nyepesi kwa wagonjwa wanaofika kupata huduma ya tiba. Duka hilo ni sehemu ya mkopo wa dawa za Sh milioni 50 kutoka MSD.

Duka hilo lilianzishwa kwa mtaji wa Sh milioni nne, kwa kuanza kununua dawa muhimu na za lazima kwa wateja wa bima.

Hayo yalisemwa juzi na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Dk. Aziz Msuya  kwa viongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo, waliofika kuangalia shughuli zinazofanywa hospitalini hapo.

Alisema duka hilo ni utekelezaji wa agizo la Serikali Kuu za kuzitaka hospitali na vituo vya afya kuwa na duka la dawa, na kwamba tayari wameshailipa MSD kiasi hicho cha fedha kupitia duka hilo la jamii, lililobadilishwa kutoka duka la dawa la bima na kuwa la jamii.

“Duka hili linalotoa huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya limekuwa kivutio kwa wateja wengine wa kawaida waliokosa dawa kwenye duka la utaratibu wa kawaida, ambalo linasaidia wananchi waliokuwa wananunua dawa nje.

“Mpaka sasa kupitia duka la bima, huduma za afya zimeimarika kwani dawa zinapatikana kwa asilimia 97, ambapo fomu zilizokuwa zinatoka nje zimepungua, na kwa baadhi ya siku kutokuwepo kabisa sanjari na upatikanaji wa uhakika wa dawa,” alisema Dk. Msuya.

Aidha  alisema kuwa mapato yameimarika kutoka Sh milioni nne wakati wanaanzisha duka hilo hadi Sh milioni 85 ikiwa ni mafanikio makubwa, ukilinganisha na mapato ya fomu ya bima ya afya za madai yakiwa Sh milioni 20 kwa mwezi wakati mwingine kushuka hadi Sh milioni 17 kutokana na kukosekana kwa dawa.

Kwa upande wake, Mratibu wa Bima ya Afya Wilaya ya Bagamoyo, Dk. Jane Mcharo, alisema kuwa uwepo wa duka hilo umeongeza mapato ya bima ya afya kupitia fomu za madai kutoka Sh milioni 35 au zaidi kwa mwezi na mapato taslimu katika duka pekee kufikia Sh milioni 15 kwa mwezi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles