MKONGWE wa muziki nchini, Dudu Baya, anatarajia kuachana na ukapera Januari mwakani ambapo atafunga ndoa.
Msanii huyo amedai kwamba katika maisha yake amefanikiwa kupitia mambo mengi ya ujana lakini kilichobaki kwa sasa ni kuishi maisha ya ndoa.
“Ninatarajia kufunga ndoa Januari mwakani kwa kuwa tayari nimepitia maisha mbalimbali ya ujana kilichobaki ni kukaa na familia.
“Ninaishi na mwanangu Wille na mwakani ataanza kidato cha kwanza, hivyo lazima nifunge ndoa niishi kama baba wa familia,” alisema Dudu Baya.
Msanii huyo amekaa kimya kwa muda mrefu, lakini amedai mwakani ataanza harakati za kuendeleza muziki wake.