31.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 19, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

DRC yatoa Saa 48 kwa Rwanda kusitisha shughuli za Kidiplomasia

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) imeiagiza Rwanda kufunga shughuli zake zote za kidiplomasia na kibalozi nchini humo ndani ya saa 48. Hatua hiyo imeonekana kama mwendelezo wa mvutano unaoongezeka kati ya mataifa hayo jirani.

Tangazo hilo linakuja wakati kundi la waasi wa M23, linalohusishwa na jamii ya Watutsi, likiendelea na mashambulizi makubwa katika mji wa Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini.

Kwa muda mrefu, mamlaka ya Kongo pamoja na wataalam wa Umoja wa Mataifa wamekuwa wakiishutumu Rwanda kwa kuunga mkono waasi wa M23, madai ambayo Kigali imekanusha mara kwa mara.

Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya DRC ilisema, “Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imejitolea kuheshimu taratibu zote za kidiplomasia na kuhakikisha mabadiliko ya utaratibu wa uamuzi huu.” Aidha, DRC imewaita wanadiplomasia wake walioko Kigali kurejea mara moja. Mpaka sasa, Rwanda haijatoa tamko rasmi kuhusu hatua hiyo ya DRC.

Uamuzi huu wa DRC unafuatia kuuawa kwa Gavana wa kijeshi wa Kivu Kaskazini siku ya Alhamisi, mauaji yanayodaiwa kufanywa na waasi wa M23. Aidha, katika mashambulizi yao ya karibuni, waasi hao wamewaua wapiganaji wasiopungua 12 wa kigeni na kuendelea kusababisha maafa makubwa kwa raia wa eneo hilo.

Wakati huohuo, Uturuki imejitolea kuwa mpatanishi wa mzozo baina ya DRC na Rwanda. Hata hivyo, viongozi wa Kongo wamekataa pendekezo hilo, wakisisitiza kuwa, “Suluhisho za Kiafrika lazima zipatikane na Waafrika.”

Hali ya mvutano kati ya DRC na Rwanda inaendelea kuibua wasiwasi mkubwa wa kiusalama, huku jumuiya za kimataifa zikihamasishwa kushiriki kwa dhati katika kutafuta amani ya kudumu mashariki mwa DRC.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
594,000SubscribersSubscribe

Latest Articles