Drama ya kusisimua ndani ya startimes

0
1262

Kampuni ya ving’amuzi ya Startimes kupitia channel yake ya St Novela E imedhamiria kuwapa burudani wateja wa king’amuzi hicho kwa kuonesha filamu ya Kifilipino ijulikanayo kama “The General’s Daughter” yenye kisa cha kusisimua.

Startimes itarusha filamu hiyo kuanzia tarehe 25 Machi, kila siku kuanzia Jumatatu mpaka Jumapili saa 3 Usiku kwenye Chaneli ya ST Novela E. Ili uweze Kupata burudani hiyo yapaswa kulipia sasa kifurushi cha king’amuzi chako ili ushuhudie Drama hiyo.

Drama ya The General’s Daughter inazungumzia binti wa Kifilipino aitwaye Rhian ambaye ni nesi katika jeshi la nchi hiyo, bila kufahamu anafundishwa mbinu za kipelelezi na kijeshi kumuangamiza baba yake mzazi bila yeye kujua.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here