25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Drake amjibu shabiki Nigeria

NEW YORK, MAREKANI

HATIMAYE rapa Aubrey Graham maarufu kwa jina la Drake, amejibu ombi la shabiki wake nchini Nigeria ambaye alitumia ukurasa wake wa Instagram na kumuomba amfanyie mpango siku moja apande ndege na kwenda Marekani kumuona msanii huyo.

Shabiki huyo pia ni mwanafunzi wa chuo cha TASUED nchini Nigeria, hivyo wiki iliopita aliposti video yake akiimba wimbo wa Drake na kisha kuomba amfanyie mpango wa kupanda ndege.

Drake hakuchelewa, alimjibu na kumwambia hasiwe na wasiwasi akae tayari kwa ajili ya safari hiyo, lakini itakuwa moja kwa moja kwenda kuitazama moja ya shoo yake.

“Wala usiwe na wasiwasi, jiandae kwa ajili ya safari ya kuja kutazama shoo yangu,” alijibu Drake na kisha akaamua kumfolo moja kwa moja kijana huyo kwenye ukurasa huo wa Instagram.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles