-Kinshasa
Mamlaka za afya nchini DR Congo zimetangaza kuanza kampeni ya chanjo ya dhidi ya mapamabano ya ugonjwa wa Covid 19 nchini humo kuanzia leo tarehe 19 Aprili kwa kutumia chanjo ya Oxford / AstraZeneca.
Zoezi la chanjo litakuwa la hiari na watakaopewa kipau mbele ni wafanyikazi wa huduma za afya, watu walio katika mazingira magumu walio na magonjwa sugu, na wale walio katika hatari kwa sababu ya kazi yao.
Kikosi kazi cha mapambano dhidi ya Covid-19 kimewahakikishia umma kuwa dozi ya chanjo ya AstraZeneca ipo milioni 1.7, ambazo zilifikishwa Kinshasa mapema Machi, ni salama kwa matumizi.
Mnamo Machi 12, DR Congo iliahirisha uzinduzi wa kampeini yake chanjo ya Covid-19, iliyopangwa kufanyika Machi 15, kama hatua ya tahadhari kufuatia hofu katika mataifa mengine kuhusu usalama na ufanisi wa chanjo ya AstraZeneca.