29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

DP yatilia shaka kifo cha Mtikila

chrNA TUNU NASSOR, DAR ES SALAAM

UONGOZI wa Chama Cha Demokratic (DP), umesema una shaka na mazingira ya ajali iliyosababisha kifo cha mweyekiti wa chama hicho, Mchungaji Christopher Mtikila.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwa marehemu Mikocheni Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu wa DP, Abdul Mluya alisema kuna mambo yanashitusha namna tukio zima lilivyotokea.

Alisema kuna picha zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii, zikionesha jinsi Mtikila alivyopata ajali.

“Tukio hili lilitokea ghafla na ilikuwa alfajiri, nani aliyejiandaa kupiga picha zikionesha jinsi alivyopata ajali na kuzisambaza katika mitandao ya kijamii kwa muda ule….nijambo la kujiuliza,” alisema Mluya.

Alisema tangu marehemu Mchungaji Mtikila azungumze na waandishi wa habari hivi karibuni, alikuwa akifuatiliwa na kutishiwa mara kwa mara.

“Hivi karibuni tulifanya mkutano Bunda mkoani Mara, tulipoondoka tuliona gari ikitufuatilia, tulipofika Serengeti Mchungaji Mtikila alilaza kiti na kufunga mkanda, huku akimwambia dereva aendeshe kwa kasi anavyoweza kukimbia,” alisema Mluya.

Alisema anaiomba Serikali na vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hilo.

Naye msemaji wa familia, Victor Manyahi alisema mwili wa marehemu Mtikila utaagwa leo katika viwanja vya Karimjee saa 3 asubuhi na kusafirishwa kwenda kijijini kwao Milo, Ludewa mkoani Njombe kwa mazishi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles