26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Dondoo.

Barca wateta na Haaland.

UONGOZI wa Barcelona umetajwa kuanza mazungumzo na wawakilishi wa staa wa Borussia Dortmund, Erling Braut Haaland.

Wakati huo huo, inaelezwa kuwa Dortmund wameendelea kusisitiza kuwa nyota huyo raia wa Norway hauzwi ng’o.

CHANZO: Eurosport

STERLING AWEKWA SOKONI CITY

MANCHESTER City wako tayari kumpiga bei mshambuliaji wake raia wa England, Raheem Sterling.

Sterling (26), anauzwa ili ipatikane fedha ya kumsajili Erling Braut Haaland na ‘mido’ wa Aston Villa, Jack Grealish.

CHANZO: Football Insider

NEYMAR KURUDI LA LIGA?

BARCELONA wameanza mazungumzo na mabosi wa PSG kuona kama watawashawishi kumwachia Neymar.

Hata hivyo, hivi karibuni Neymar alisema anakaribia kusaini mkataba mpya pale PSG.

CHANZO: Sport

CHELSEA WAMTAKA RABIOT

CHELSEA wameanzisha harakati za kuisaka saini ya kiungo wa Juventus anayetakiwa Barcelona, Adrien Rabiot.

Lakini sasa, Juve watakuwa tayari kumwachia Mfaransa huyo endapo watawekewa mezani Pauni milioni 17.

CHANZO: Calciomercato

JUVE KUMRUDISHA ALLEGRI

UONGOZI wa Juventus unaangalia uwezekano wa kumrejesha kwenye benchi la ufundi kocha raia wa Italia, Massimiliano Allegri.

Kwa mujibu wa taarifa, Juve wanamuona Allegri kuwa atafaa kuchukua nafasi ya kocha anayeboronga, Andrea Pirlo.

CHANZO: Gazzetta dello Sport

VIDAL AKWAMA INTER KISA MKWANJA

KLABU ya Inter Milan inashindwa kumsajili Arturo Vidal kwa kuwa kiungo huyo anataka mshahara mkubwa.

Inter wanataka kumchukua nyota huyo wa Marseille mara tu dirisha kubwa la usajili litakapofunguliwa.

CHANZO: Calciomercato

VAZQUEZ KUPEWA MKATABA MADRID

REAL Madrid wanakaribia kumpa mkataba mpya mshambuliaji wake raia wa Hispania, Lucas Vazquez.

Madrid wanataka kufanya hivyo licha ya Vazquez mwenye umri wa miaka 29 kuwindwa na Bayern Munich na PSG.

CHANZOP: AS

MESSI MKATABA MIAKA 10

LIONEL Messi atapewa mkataba wa miaka 10 ili kuendelea kuitumikia klabu yake ya Barcelona.

Taarifa hiyo imekuja baada ya baba yake Messi kukutana na Rais wa Barca, Joan Laporta.

CHANZO: TV3

HUYU AKILI YOTE LIVERPOOL

KIUNGO wa Borussia Monchengladbach, Florian Neuhaus, anasubiri kwa hamu kujiunga na Liverpool mwishoni mwa msimu huu.

Imeelezwa kuwa Neuhaus anatamani kuona akihamia Liver, licha ya kwamba M’gladbach wanataka Pauni milioni 34.

CHANZO: Bild

SPURS WAMTEMA RODGERS

KLABU ya Tottenham imepotezea rasmi mpango wa kumwajiri kocha wa Leicester City, Brendan Rodgers.

Uamuzi wa Spurs umekuja baada ya kubaini watalazimika kutumia Pauni milioni 70 kumng’oa Leicester.

CHANZO: The Sun

CAVANI KUONGEZA MWAKA UNITED

IMERIPOTIWA kuwa mkongwe Edinson Cavani, ataongeza miezi 12 ya kuendelea kuitumikia safu ya ushambuliaji ya Manchester United.

Huku mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi ujao, zilikuwapo tetesi kuwa angetimkia Boca Juniors.

CHANZO: ESPN

JUVE WAMPIGIA HESABU BRUNO

VIGOGO wa Serie A, Juventus, wanavutiwa na saini ya kiungo anayeibeba Manchester United kwa siku za hivi karibuni, Bruno Fernandes.

Licha ya kwamba mkataba wa Bruno utakwisha mwaka 2025, hilo haliitishi Juve iliyopania kumsajili kupitia dirisha kubwa la mwaka huu.

CHANZO: Calciomercato

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles