30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Dola milioni 11.9 kutumika mapambano dhidi ya VVU

AMINA OMARI -TANGA

SHIRIKA la Amref Health Africa linatarajia kutumia Dola za Marekani milioni 11.9 kwa mwaka wake wa kwanza wa utekelezaji wa mradi wa matibabu ya kufubaza virusi vya ugonjwa wa Ukimwi katika mikoa ya Tanga na Zanzibar.

Mradi huo ujulikano kwa jina la Afya Kamilifu unatarajiwa kutekelezwa hapa nchini kwa miaka mitano (2018-2022) huku ukiwa umelenga katika kusaidia kumaliza janga la Ukimwi ifikapo mwaka 2030.

Akizindua mradi huo mkoani hapa jana, Mkuu wa Mkoa, Martine Shigela alisema umekuja wakati mwafaka ambao Serikali ipo katika mikakati ya kuhakikisha wanapunguza maambukizi ya ugonjwa huo na kwa wale walioathirika kuanzishiwa tiba mara moja.

“Licha ya juhudi kubwa zinazochukuliwa na Serikali ikiwamo kusambaza dawa za ARV katika vituo vya afya, bado mwitikio ni mdogo kwa waathirika kuzitumia, hivyo naamini kupitia mradi huu tutaweza kuwaunganisha wananchi wengi katika kupatiwa huduma za matibabu,” alisema.

Mkurungenzi Mkazi wa shirika hilo, Dk. Florence Temu alisema mradi huo unalenga kuongeza idadi ya watu wanaojijua kuwa wanaishi na VVU na Ukimwi na wanapatiwa huduma za upimaji, matunzo na matibabu ya kufubaza virusi hivyo.

“Hadi kufika mwisho wa mradi tunalenga kuhakikisha kwamba watu wote wanaoishi na VVU na Ukimwi mkoani hapa watakuwa wanajua hali zao na wanapatiwa matibabu,” alisema Dk Temu.

Hata hivyo, Mkurungenzi wa mradi wa Afya Kamilifu, Dk. Edwin Kilimba alisema mradi huo utaimarisha ufuatiliaji na tathmini ya taarifa za hali halisi za maendeleo katika muda halisi pamoja na kuimarisha mifumo ya usimamizi wa data kuanzia ngazi ya kituo cha afya hadi mkoa.

“Kupitia mradi huu utaweza kusaidia vituo vya afya uwezo wa umiliki wa data na usimamizi bora wa data na matumizi yake kuanzia ngazi ya kituo chenyewe na wilaya ili kuongeza ubora wa huduma kupitia timu ya usimamizi wa afya ngazi ya mkoa,” alisema Dk. Kilimba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles