26.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 26, 2022

DMX: NAKARIBIA KUMRUDIA MUNGU

NEW YORK, MAREKANI


NYOTA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Earl Simmons, maarufu kwa jina la DMX, amedai kuwa, anakaribia kumrudia Mungu kutokana na kukumbwa na mikasa mbalimbali katika maisha yake.

Msanii huyo mwaka juzi alifungwa jela kwa kushindwa kuhudumia watoto wake 15, lakini baada ya kutoka jela aliongeza mtoto mwingine wa 16. Hata hivyo, anadai kwamba amekuwa katika wakati mgumu miaka ya hivi karibuni.

“Siku zote maisha yanabadilika, kuna wakati nimekuwa nikifurahia maisha yangu, lakini wakati mwingine nakumbwa na matatizo mbalimbali.

“Nadhani wakati unakaribia wa kumrudia Mungu wangu ili baadhi ya mambo yaende sawa, afya yangu haijakaa sawa na nimeshindwa kufanya onyesho California mwishoni mwa mwiki iliyopita, lakini ninaamini nikikaa sawa nitawaburudisha mashabiki wangu,” alisema DMX.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
176,803FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles