25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Dkt. Kimei aahidi kukamilisha ahadi zake

Upendo Mosha, Moshi

MBUNGE wa jimbo la Vunjo, mkoani Kilimanjaro,Dk. Charles Kimei, amewahakikishia wananchi kutekeleza kwa vitendo  ahadi zote alizoziahidi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba mwaka 2020 ikiwemo upatikanaji wa halmashauri mpya ya jimbo hilo.

Dkt.Kimei aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wananchi mara baada ya kutembea na kukagua mradi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Njiapanda,wilayani Moshi mkoani hapa.

Alisema atahakikisha ahadi zote alizozitoa katika uchaguzi mkuu zinatekelezwa kwa vitendo ikiwa ni pamoja na kufatilia ahadi zote zilizotolewa na Hayati Dk.John Pombe Magufuli kwa lengo la kuleta imani kwa wananchi na kuiamini serikali.

“Nitaendelea kufuatilia kwa karibu ahadi zangu binafsi, ahadi za hayati Dk. Magufuli pamoja na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi (CCM) 2020-2025 kwa karibu ili kuhakikisha nakidhi matarajio na matumaini makubwa ya wananchi waliyokuwa nayo wakati wanaichagua CCM katika uchaguzi mkuu Oktoba, 2020″alisema

Aidha alisema anaendelea kufuatia suala la kupatikana kwa halmashauri mpya ya jimbo la vunjo ambayo iliombwa toka mwaka 2000 bila mafanikio na kwamba upatikanaji wa Halmashauri hiyo mpya utaharakisha mchakato wa maendeleo kwa wananchi.

“Mchakato wa kisheria kwa mujibu wa muongozo wa TAMISEMI wa kupandisha hadhi maeneo ya kiutawala tayari umeanza ambapo hoja binafsi iliwasilishwa kuhusu kuanzishwa kwa halmashauri ya wilaya ya Vunjo, ikapokelewa na kuungwa mkono na madiwani wote 42 wa halmashauri ya wilaya ya Moshi hivyo tujipe muda naendelea kushughulikia”alisema

 “Taarifa hiyo iliwasilishwa kwenye baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Moshi na ilipokelewa na kuungwa mkono kwa asilimia mia moja kwa sasa hatua zinazofuata ni taarifa hizo kuwasilishwa kwenye baraza la ushauri la wilaya (DCC), baraza la ushauri la mkoa (RCC) na baadaye wizara ya TAMISEMI kwa hatua zaidi”alisema Dk.Kimei

Hata hivyo Mbunge wa jimbo la Vunjo Mhe Dkt Kimei aliwataka wananchi kuendelea kuwa watulivu kwani tayari Mhe Rais Samia Suluhu Hassan amekwishasema ahadi zote zilizotolewa na hayati Magufuli serikali anayoiongoza itazitekeleza kikamilifu.

Akizungumzia ujenzi wa mradi huo wa vyumba vya madarasa,alisema kiasi cha milioni 60 zimekwisha tolewa kutoka katika mfuko wa lipa kulingana na matokeo EP4R  kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa  madarasa, maabara, mabweni, nyumba za walimu na matundu ya vyoo.

“Mradi huu unaendelea kukamilika lakini miradi ya zahanati, vituo vya afya, miundombinu ya umwagiliaji, usambazaji umeme vijijini, uchongaji na ukarabati wa barabara, ujenzi wa vivuko, madaraja, uboreshaji wa miundombinu ya maji safi na salama hii yote ipo katika hatua mbalimbali na mimi binafsi nimekuwa nikipita kuikagua”alisema

Abel Msuya, mkazi wa njiapanda, alimshukuru Rais Samia Hassan Suluhu  kwa kurejesha mahusiano na Kenya hali iliyopelekea kufunguliwa kwa mpaka wa Holili na sasa biashara ya mazao inafanyika vizuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles