24.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Dk. Yonazi ateta na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dk. Jim Yonazi akutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Dk. Germana Leyna kwa lengo la kumpitisha katika majukumu yanayohusu taasisi hiyo ikiwa ni sehemu ya ratiba ya Katibu Mkuu huyo kujengewa uelewa kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Idara na Taasisi zilizochini ya Ofisi yake.

Mtendaji Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt.Germana Leyna akieleza utendaji wa taasisi yake wakati wa kikao chake na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dk. Jim Yonazi (hayupo pichani) hii leo Machi 10, 2023.

Kikao hicho kilifanyika Machi 10, 2023 katika ofisi yake jijini Dodoma na kueleza kuwa ofisi yake itaendela kutoa ushirikiano kwa taasisi hiyo kuhakikisha masuala ya lishe yanapewa kipaumbele nchini na yanaratibiwa kwa matokeo chanya.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dk. Jim Yonazi akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Dk. Germana Leyna alipokutana naye machi 10, 2023 kwa lengo la kufahamiana na kujua majukumu ya Taasisi hiyo.Kikao kilifanyika katika Ofisi yake iliyopo Mtaa wa Relini jijini Dodoma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,213FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles