26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

DK TULIA, MDEE WAONGOZA WAOMBELEZAJI MAZIKO YA DIWANI

Na PENDO FUNDISHA-MBEYA

NAIBU Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson jana aliongoza mamia ya wakazi  wa Mkoa wa Mbeya  kushiriki mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Viti Maalumu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Esther Mpwiniza.

Mbali na Dk Tulia, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa, (BAWACHA)  Halima Mdee alishiriki mazishi hayo na kueleza kuwa chama kilivyopata pigo kutokana na kifo cha Esther, kutokana na mchango wake wa maendeleo kwenye ndani ya chama na kwa jamii nzima ya watanzania.

Katika mazishi hayo, yaliyofanyika jana eneo la makaburi la Saba Saba Jijini hapa, wananchi mbalimbali hususani wafuasi wa chama hicho walijitokeza kwa wingi kushiriki mazishi ya mpiganaji huyo ambapo kifo chake kinatajwa kwamba kimetokana na shinikizo la damu .

Katika salamu zake Mdee alielezea jinsi chama kilivyopata pigo kutokana na msiba huo. Alisema marehemu alikuwa  na mchango  mkubwa  wa maendeleo ndani ya chama na kwa jamii nzima ya watanzania.

Alisema umefika wakati ambao asiwepo raia wa Tanzania ambaye uhai wake utakatishwa kwa kupigwa risasi kama ilivyotokea jaribio la Mbunge wa Singida Mashariki,Tundu Lissu (Chadema) ambaye yupo nchini Kenya kwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.

Kwa upande wake, Mbunge wa  Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Chadema), alimpongeza Dk. Tulia kwa kitendo chake cha kushiriki mazishi ya kada huyo huku akikitaka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuweka itikadi za vyama pembeni wakati wa matatizo.

“Msiba hauna itikadi, napenda salamu hizi zifike ndani ya CCM na Serikali kwa ujumla iache kuwazuia wananchi kushirikiana misibani,”alisema Sugu.

Kabla ya kukumbwa na mauti, Diwani Mpwiniza  aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema Wilaya ya Mbeya kwa kipindi cha miaka sita.

Pia alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Fedha katika Baraza la Halmashauri Jiji la Mbeya, Mjumbe wa ALAT Mkoa na Mwenyekiti wa madiwani wanawake Wilaya ya Mbeya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles